Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari, Wema bifu liendelee, lisindelee

Zari Pic Data Zari, Wema bifu liendelee, lisindelee

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

IMEKUWA wiki ya majibizano kati ya mjasiriamali Zarina Hassan ‘Zari’ na mrembo Wema Sepetu.

Wawili hao ambao wamewahi kuwa katika mahusiano na msanii Diamond Platnumz kwa nyakati tofauti ni paka na chui. Hii inawapa tofauti kati yao na Hamisa Mobetto na Tanasha Donna ambao licha ya wote kuzaa na msanii huyo kwa sasa ni marafiki hadi wanashoneana nguo.

Wiki iliyopita Zari na Wema walianzisha upya bifu kwa kujibizana huko mtandaoni, chanzo kikubwa ikiwa ni ile ishu ya kupotea kwa mbwa wa Wema anayeitwa Vanilla Manunu.

Aliyeanza uchokozi ni Zari na ni baada ya shabiki mmoja mtandaoni Machi, mwaka huu kumuuliza mama huyo kama amemuona mbwa wa Wema huko Sauzi ambapo majibu yake yalikuwa “nbwa amefichwa ndani ila wanafanya kiki tu.”

Katika kipindi chote hicho, Wema aliamua kukaa kimya kwani ni muda ambao kulikuwa na msiba wa Rais John Magufuli na serikali kutangaza siku 21 za maombolezo.

Hata hivyo, mara baada ya kuupumzisha mwili wa Dk Magufuli, Wema akaibuka na andiko lake lililosomoka hivi. “Ok mimi sio kama yeye, I dont need kik to survive, nguvu anazotumia yeye mimi situmii.”

Wiki iliyopita akiwa katika uzinduzi wa tamhiliya ya ‘We Men’, waandishi wa habari walimchokonoa tena Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 kwa kumuuliza alijisikiaje Zari alivyoandika kuhusu suala la Manunu (mbwa wake) kuwa ilikuwa ni kiki.

Wema alisema kuwa: “Unajua ukiwa mwizi unahisi kila mtu mwizi, ukiwa muongo unahisi kila mtu muongo na ukiwa mtu mhuni utahisi kila mtu mhuni, so pigia mstari.”

Mashabiki wachonganishi hawakuyakaushia majibu hayo ya Wema na kumpasia tena Zari ambapo shabiki anayejulikana kwa jina la Therealcathe_tz huko Instagrm alimuuliza mama huyo, “Zari wee mbwa wako hajapotea kama wa Wema, halafu Wema alikujibu vibaya Boss Lady.”

Majibu ya Zari yaliyofuata yalikuwa hivi: “Therealcathe_tz it’s Ramadhan na natoa msaada. She could use some free food, naona kabakisha kichwa tu. Hiyo ni njaa, let her eat some food she will be fine.” Wema sasa katika hili jioni yake si akaweka video akionyesha vyakula mbalimbali kwa ajili ya futari na kuandika, “kugombana na watu wazima ni kujitafutia laana... Na mimi nina heshima sana kwa wakubwa zangu... pia ni mskivu...nafanyia kazi ushauri.” Ni bifu au wananogesha Insta?

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz