Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari: Ukipata nafasi ya kuchiti, chiti

ZARI KUCHITI Zari: Ukipata nafasi ya kuchiti, chiti

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sosholaiti ambaye ni babu mama wa msanii Diamond Platnumz ambaye ni Zari The Boss Lady ameibua mjadala mzito.

Hii ni baada ya kusema kuwa, katika nyakati za sasa wanawake wameamka na wanaweza kufanya mambo ambayo wanaume pia wanafanya.

Zari amewapa wanawake ushauri wenye utata kuwa wanapaswa kusaliti penzi lao wanapopata fursa ya kufanya hivyo kwa ajili ya pesa.

Zari alikuwa akitetea kauli yake ya wanaume wana-cheat kwa sababu za kipuuzi.

"Mtoto wa kike, ukipata nafasi ya ku-cheat kwa sababu ya pesa basi fanya hivyo. Hawa wanaume wana-cheat kwa mambo ya kijinga kama mapaja ya rangi ya kahawia, pete za ulimi na makalio makubwa. Saliti penzi kwa nyumba, saliti penzi kwa kipande cha ardhi, saliti kwa gari la ndoto yako, ndivyo lilivyo,” amesema Zari anayetajwa kuwa na utajiri mkubwa na mama wa watoto watano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live