Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari: Sijui kama Nillan wa Mobetto ni mtoto wa Diamond

Mobetto Mondi (1).png Mtoto Nillan wa Mobetto na wazazi wake.

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama watoto wa msanii Diamond Platnumz, Zarina Hassan (Zari The Boss Lady) amesema kuwa hajui kama mtoto wa Hamisa Mobetto (Prince Nilan) ni mtoto wa Diamond.

Zari amesema hana ukaribu na mtoto huyo kwa sababu hana uhakika kama yule mtoto ni wa Diamond hivyo anasubiria kuambiwa na Diamond mwenyewe kama yule ni mwanaye ili amuweke karibu na wanaye.

“Yani hapo kabisa ndiyo sijui, Diamond mwenyewe ndiyo anaweza kujielezea kama yule mtoto ni wake au sio wa kwake lakini kwa upande wangu mimi sijui… sijui… sijui… sijui… sijui kabisa.

“Akiniambia huyu ni mtoto wangu nataka ajuane na hawa wenzake nitamkaribisha lakini mpaka sasa hakuna mawasiliano rasmi baina yangu mimi nay eye kwamba yule ni mtoto wake,” amesema Zari.

Itakumbukwa kuwa, stori za Diamond kumkana mtoto yule zilisambaa mpaka Mobetto mwenyewe akadai kuwa Diamond alishawahi kupima DNA na kujiridhisha kuwa yule ni mwanaye lakini mara kadhaa Diamond amekuwa akisema kuwa mama wa mtoto huyo ndiye anajua ukweli lakini yeye hawezi kulizungumzia kwani atamharibu mtoto kisaikolojia pindi atakapokuwa mkubwa.

Imeshuhudiwa mara kadhaa watoto wote wa Diamond ambao amezaa na Zari (Latifah Dangote, Dylan Abdul Naseeb) na yule aliyezaa na Tanasha Donna, Naseeb Jr wakijumuika kwenye familia na mama Dangote (mama Diamond) lakini Nilan amekuwa akikosekana kwenye familia hiyo na kuibua maswali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live