Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari: Mimi sio shabiki wa Diamond

Zari Hj Diamond.png Zari na Diamond

Sat, 18 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zari The Boss Lady; ni baby mama wa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye anaweka wazi kwamba huwa anawasiliana na mzazi mwenzake huyo mara kwa mara.

Mara tu baada ya kutua Tanzania kwa ziara ya kikazi, Zari amesema kuwa kuna mengi ambayo hufanyika kati yake na Diamond au Mondi bila kutangaza.

Alieleza kuwa yeye na Diamond hujadialiana kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu ikiwamo namna ya kulea watoto wao wawili pamoja.

“Mimi kuonana na Diamond ama familia yake siyo lazima iwe kwenye vyombo vya habari, tumeshakuwa familia, mimi naongea na Diamond kila wakati kuhusu watoto na jinsi ya kuwalea.

“Siyo lazima nikikutana naye niposti, mimi siyo shabiki wake, mimi ni mama wa watoto wake,” anasema Zari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live