Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaiylissa: Najutia kuolewa na Dulla Makabila

Makabila Sersss Zaiylissa: Najutia kuolewa na Dulla Makabila

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mke wa Dulla Makabila, Zaiylissa amesema kuna sehemu anajutia kuolewa na Staa huyo wa Singeli Bongo.

Akizungumza katika podcast ya Lil Ommy, Zaiylissa amesema kwa namna moja au nyingine kuvunjika ndoa hiyo kumemtia doa kama mwanamke.

“Najutia hata kwanini niliolewa naye, hainitesi ila kuna muda ni kama kuharibiana CV. Unajua mimi nilishaolewa mara ya kwanza, kwa hiyo alivyonioa yeye nikasema nitahidi hii niwa-prove watu wrong.” amesema.

“Unajua ikitokea ndoa kuvunjika anayeonekana mbaya ni mwanamke, bila kujua nini kimetokea ila mbaya ni mwanamke.” amesema Zaiylissa.

Zaiylissa ameendelea kwa kusema, “Inaonekana ameolewa mara ya kwanza, ameolewa mara ya pili, ana shida gani?, watu hawajui umepitia nini au nini kimetokea, wanakuona wewe ndio una shida.

Utakumbuka kuwa Zaiylissa anayefanya vizuri katika tamthilia ya Jua Kali, aliolewa na Dulla Makabila Julai mwaka huu ikiwa ni ndoa ya pili kwa Makabila pia.

Dulla alifunga ndoa na Rahima Mei 2021 ikiwa ni ndoa yake ya kwanza lakini nayo haikuweza kudumu.

Katika Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day mwaka 2022, Makabila alichora tattoo ya mkewe, Rahima.

“Hakuna cha zaidi, ni kwa sababu nampenda na ni mke wangu, niliona hiyo ni zawadi ambayo naweza kumpa Siku ya Wapendanao na alifurahi.” alisema Dulla Makabila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live