Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahara amekwenda kutengeneza Playlist Peponi

Zahara E Zahara amekwenda kutengeneza Playlist Peponi

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nilikuwa kijana sana. Workaholic. Saa 24 busy na checklist. Marejeo home kumekucha, kuuswafi mwili, kubadili nguo na kuingia ofisini asubuhi.

Zaidi ya saa 48 bila kusalimisha kiwiliwili kitandani. Miaka 10 na ushee imepita. Ujana, nishati ni super-voltage.

Misele usiku. Kuendesha gari speed kuzidi 200km kwa saa. Kumbukumbu hazifutiki. Nusura za ajali licha ya tairi za mbele kupasuka katikati ya mwendo mkali.

Mafanikio ya kazi zenyewe. Muhimu, sauti ya Zahara ikiniliwaza nilipoendesha gari usiku.

"Loliwe".

Uloliwe wayidudula

Loliwe wayidudula

Uloliwe wayidudula

Nang'esiza.

Muziki mzuri hauhitaji tafsiri ya kinachoimbwa. Ningesikiliza "Loliwe", kuanzia Dar es Salaam mpaka Bagamoyo, kisha porini kwenye kambi ya Maisha Plus. Sikuuchoka wimbo. Sikumkinai Zahara.

Sometimes ningeweka "Letter to My Unborn Child" wa Tupac au "Mysterious Girl" wa Peter Andre. Isingechukua muda ningemrudia Zahara na Loliwe. Nilifurahia kampani ya Zahara kila nilipoketi nyuma ya sterling. Loliwe ni moja ya nyimbo zangu pendwa kabisa.

Tamasha la RMB Starlight Classics 2019, Country Club, Johannesburg. Zahara akiwa na full orchestra akaperform "Phendula" kwa umahiri. Nika-fall in love with Phendula.

Zahara ana nyimbo nyingi nzuri na haziboi kusikiliza hata ukirudia mara kwa mara. Albamu tano kwenye account. Hata hivyo, kwangu, Loliwe na Phendula ni best kutoka kwake.

Jambo moja la kushuhudia kuhusu Zahara; utunzi na uimbaji wake ni ule wa kutoka moyoni, kwa hivyo inakuwa rahisi kwake kugusa nyoyo za mamilioni ya mashabiki wake duniani. Zahara ni Queen of Afro-soul.

Uzao wa Novemba 9, 1987, East London, Afrika Kusini. Akaimba kwaya kanisani akiwa na umri wa miaka sita. Nguvu ya sauti yake ikamfanya ajumuishwe kwaya ya wakubwa alipokuwa na umri wa miaka tisa.

Muziki mzuri, tuzo nyingi na mamilioni ya mashabiki, ilipofika Desemba 11, 2023, akiwa na umri wa miaka 36, akaitikia wito wa Mungu.

Maisha baada ya kifo yamesajili binadamu mwenye kipaji kupindukia. Pengine ametangulia kutengeneza playlist itakayoburudisha watu wa peponi. Nikifuzu pepo, nitaomba Zahara a-perform Loliwe na Phendula ili aniburudishe na wenzangu.

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live