Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zabibu Kiba amtapika Issa Azam,"asilazimishe undugu"

Zabibu Kiba Zabibu Kiba amtapika Issa Azam,

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zabibu Kiba; ni dada wa Mfalme wa Bongo Fleva, King Kiba ambaye kwa mara ya kwanza amejitokeza hadharani na kumtapika jamaa aitwaye Issa Azam anayesema ni mtoto wa mama mdogo wa Kiba.

Zabibu anaonesha kushangazwa na madai ya Issa Azam ya kila mara kuwa King Kiba ni ndugu yake.

Zabibu amefunguka kuwa kaka yake, King Kiba amezaliwa na kusomea jijini Dar na siyo mkoani Kigoma kama inavyoaminiwa.

Zabibu amewataka waandishi wa habari kumuuliza Issa Azam ana undugu gani na King Kiba?

Zabibu amesema; “Hivi ni lazima mtu kulazimisha undugu na mtu jamani? Kila ukihojiwa mi ndugu wa f’lani kwa undugu upi hasa? Hebu tupishe bwana, ongea matatizo yako uliyokuwa nayo au unashindwa tukusaidie kuyaongea, ushindwe na uache kumuongelea mtu.

“Mnalazimisha sasa kama ana undugu na sie upi, awaoneshe ushahidi, sasa mnadanganywa kila siku mnakubali nyie.

“Ali kazaliwa Dar (siyo Kigoma kama mnavyodanganywa), amekulia Dar siyo Kigoma. Amesoma Upanga kisha Moshi Secondary siyo Kigoma, bado mnalazimisha undugu, aseme ana undugu gani na sie, kwani lazima? Mbona hawatazi ndugu zake, kang’ang’ania huku bwana goo, hatuna undugu sie na mke…”

Kwa muda mrefu, Issa Azam amekuwa chawa wa msanii Diamond Platnumz huku akimponda na kumpaka matope King Kiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live