Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

ZARI: Naweza kulala kitanda kimoja na Diamond na kusitokee kitu

Zari Na Mondi Diamond na Zari

Thu, 24 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo maarufu kutokea nchini Uganda, Zarina Hassan maarufu kama Zari ambaye ni mama wa watoto wawili wa staa wa bongo fleva, Diamond Platnumz anasema anaweza share kitanda kimoja na Diamond bila kugusana.

Zari amefunguka kuhusiana na mahusiano yake ya sasa na Diamond katika kipindi cha ''Young, African and Famous'' kwa kusema ana mahusiano mazuri na Diamond kama wazazi na sio wapenzi kama zamani na kukazia kwamba anaweza lala nae kitanda kimoja bila kugusana.

“Mimi na yeye tuna uhusiano mzuri. Mimi na Diamond tunaweza kulala kitanda kimoja, lakini hakuna kugusana”

Yeye na Diamond wanashirikiana kama wazazi kulea watoto wao na kila mmoja anaruhusiwa kuwa na mahusiano yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live