Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yvonne Chaka Chaka fundi wa muziki aliyeisimamisha Afrika

Yvonne Chaka Chaka Yvonne Chaka Chaka fundi wa muziki aliyeisimamisha Afrika

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yvonne Chaka Chaka alizaliwa 1965 Dobsonville Soweto nchini Afrika Kusini. Ni msanii mkubwa kutoka bara la Afrika na miongoni mwa wanawake 100 bora duniani wenye ushawishi zaidi.

Yvonne ni msanii wa kiafrika wa kwanza kuonekana kwenye Runinga huko Afrika kusini 1981 kupitia kipindi cha Sugar Shack ambacho kilikuwa maalumu kwa watu wenye vipaji tuu.

Phil Hallis wa Dephon Records ndiye aliyeongeza juhudi za kumwinua alipo muona huko Johannesburg wakati Album yake ya "I'm in Love with a DJ" ilipouza nakala elfu 35,000.

Yvonne ni msanii msomi akiwa na Shahada mbili alizozipata kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Kusini.

Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni;

1. Burning Up

2. Who's the Boss

3. Mother land

4. Thank You Mr DJ

5. Yvonne and Friends

6. Kwenzenjani

7. Let Him Go.

Wimbo upi unaukubali zaidi kutoka kwa mtaalamu Yvonne Chaka Chaka na unakumbuka wapi ukisikia nyimbo zake.

Dondosha watu waone umbali ulikokuwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live