Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yusuph Mlela asema hana uhusiano wa kimapenzi na Ebitoke

72091 Pic+mlela

Tue, 20 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania, Yusuph Mlela amekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji mwenzake, Ebitoke licha ya msichana huyo kudai ni wapenzi.

Kupitia mitandao ya kijamii na mahojiano kadhaa aliyofanya Ebitoke amekuwa akieleza kuwa yeye na Mlela ni wapenzi kutokana na anavyomtimizia mahitaji yake.

Picha za mastaa hao wa maigizo zinazowaonyesha wakiwa pamoja katika maeneo tofauti ndio zilizoibua  uvumi mitandaoni kuwa ni wapenzi.

Leo Jumatatu Agosti 19, 2019 Mwananchi limezungumza na Mlela na kubainisha kuwa msichana huyo ni rafiki yake kama ilivyo kwa wasanii wengine.

Ameeleza kuwa picha zinazosambaa mitandaoni wamezipiga katika kazi za sanaa.

“Ebitoke ni msanii mwenzangu nimekuwa shabiki wake wa muda mrefu kutokana na kazi zake,  tulivyokutana kwenye kazi tulipiga picha ni hivyo tu, hatuna mahusiano yoyote,” amesema Mlela.

Pia Soma

Hata hivyo, amesema Ebitoke kutangaza kuwa ana uhusiano naye hampi shida kwa kuwa anajua wao ni marafiki wa kawaida.

"Kungekuwa na jambo hata mpenzi wangu angeleta shida, lakini pamoja na Ebitoke kusema hivyo mara kadhaa haijaleta shida kwa sababu mpenzi wangu anajua ninafanya naye kazi na hakuna kingine,” amesema Mlela.

Chanzo: mwananchi.co.tz