Rapa Young Thug amerejea na albam yake mpya ya kwanza tangu Oktoba 2021.
Album hiyo inayoitwa Business Is Business limewashirikisha mastaa kama Drake, Future, 21Savage, LilGotit, YakGotti, TravisScott, Bslime na NateRuess huku MetroBoomin ndiye mtayarishaji mkuu wa albam hiyo.
BusinessIsBusiness ni Project wa kwanza ya YoungThug tangu yeye, Gunna, Deamonte "Yak Gotti" Kendrick na wanachama wengine wa kikundi cha Young Stoner Life (YSL) kukamatwa kwa mashtaka yanayohusiana na genge huko Georgia.
Young Thug alishtakiwa katika shtaka kuu la mahakama kwa kushiriki katika shughuli za genge la uhalifu mitaani na kula njama ya kukiuka Sheria ya Georgia's Racketeer Influenced and Corrupt Organizations (RICO).
Aidha alishtakiwa kwa makosa yanayohusiana na madai ya kumiliki dawa za kulevya na silaha.