Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Young Killer asogeza albamu yake mbele

Killer Pic Data Young Killer asogeza albamu yake mbele

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msanii Young Killer ametangaza kusogeza mbele kuachia albamu yake.

Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni  Erick Msodoki, ameyaeleza hayo leo Jumanne, Machi 302021 kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.

Mwaka jana msanii huyo alitangaza kuwa angeachia albamu yake Aprili  13, 2021.

Kupitia ukurasa wake huo ameandika "Napenda kuwatangizia kuwa nimehairisha kutoka kwa albamu yangu kama nilivyoahidi mwaka jana kuwa albamu hiyo ingetoka taeher 13 April 2021.  

"Kufuatia msiba wa Kitaifa wa mpendwa wetu, Hayati John Magufuli ,natangaza kuwa albamu i yenye viwango vya juu kabisa, imesogezwa mbele mpaka hapo tarehe husika nyingine itakapo tangazwa.

Ameongeza "Najua wapenzi wa mziki wangu na mashibiki zangu mlingojea sana kwa hamu lakini najua kuwa nina watu wanao nipenda sana na wako tayari kuningojea.

Hivyo basi tutaanza kuachia project hivi karibuni na ninaahidi kuwafurahisha na kukata kiu yenu kwa kila kazi itakayotoka.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz