Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Young Killer ajivunia ndoto zake kimuziki kutimia

Young Killer Msodoki Young Killer ajivunia ndoto zake kimuziki kutimia

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa HipHop nchini Young Killer Msodoki ameshare ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na video ya jinsi watu walivyohudhuria kwenye uzinduzi wa album yake, na amesema hii imempa faraja sana huku akisema ndoto yake imitimia aliyokuwa akiota siku moja aje kufanya Show yake mwenyewe akiwa kama muandaaji na mtumbuizaji pia.

Ni miaka mitatu na nusu kwa Star huyo wa Hip Hop nchini kufanya ama kutojihusisha na Show yoyote jukwaani mpaka alipofanya mara hii show ya uzinduzi wa album yake.

Hivyo ametangaza tour ambayo ataifanya baada ya hii kama moja ya njia ya kukutana na mashabiki zake sehemu tofauti tofauti nchini ambao hawajamuona kwa miaka 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live