Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Young Killer aahirisha kuachia albamu

F38d8e9b817b93e7490af703d518d870.jpeg Young Killer aahirisha kuachia albamu

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa HipHop, Erick Msodoki ‘Young Killer’ amesema kameamua kuahirisha kuiachia albamu yake iliyotarajiwa kuachiwa mwezi ujao kufuatia msiba wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli.

"Napenda kuwatangazia kuwa nimehairisha kutoka kwa albamu yangu kama nilivyoahidi mwaka jana kuwa ingetoka Aprili 13, 2021.”

“Kufuatia msiba wa kitaifa wa mpendwa wetu Rais Dk John Magufuli natangaza kuwa albamu hii yenye viwango vya juu kabisa imesogezwa mbele mpaka hapo tarehe husika nyingine itakapo tangazwa.”

“Najua wapenzi wa muziki na mashabiki wangu mlingojea kwa hamu, lakini najua kuwa nina watu wanaonipenda sana wako tayari kuningojea tena tutaanza kuachia kazi,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz