Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

YouTube watangaza ujio wa ‘Official Artist Channels’, Kilio kwa wasanii wanaotumia VEVO

1936 Dsfgft

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Mtandao wa YouTube umetangaza ujio wa kipengele kipya cha ‘Official Artist Channels’ ambayo itakuwa maalumu kwa wasanii wa muziki pekee ambao wapo kwenye mtandao huo.



YouTube wamesema kutokana na Wasanii wengi kuwa na akaunti zaidi ya moja kwenye mtandao huo wameamua kuanzisha kipengele hicho ambapo akaunti zote za msanii husika zitachanganywa na kuwa akaunti moja.

Unaweza ukajiuliza zitachanganyejwe?

Jibu ni kwamba kama msanii ana akaunti ya VEVO na ya YouTube ya kawaida akaunti hizo zote mbili zitachanganywa katika akaunti moja ya ‘Official Artist Channels’.

Kuhusu subscribers?

Subscribers wote waliopo kwenye channel mbili watajumlishwa kwenye akaunti moja ya “Official Artist Channels” automatically na watatarifiwa kwa njia ya email baada ya YouTube kumuhamisha msanii husika.

Kwanini YouTube wamechukua maamuzi hayo? 

Sababu kubwa ni ushindani wa kibiashara na VEVO, kama umekuwa mfuatiliaji wa mtandao wa VEVO ambao ni marafiki wa kibiashara na Youtube wamekuwa wakikua zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda ile hali wanafanya kazi chini ya mtandao wa YouTube kwa nchi ambazo VEVO hawapatikani.

Hata ukiangalia idadi kubwa ya akaunti za Wasanii wenye subscribers wengi duniani, kati ya Channels za YouTube na VEVO utagundua akaunti nyingi za Wasanii waliopo VEVO zimefuatwa na watu wengi zaidi kuliko zile za YouTube.

Hata kwenye nchi ambazo mitandao yote miwili yaani VEVO na YouTube inafanya kazi kama Marekani, Ujerumani, Uingereza n.k, bado Wasanii wengi wanatumia mtandao wa VEVO kitu ambacho kibiashara YouTube wanapoteza wateja wengi zaidi licha ya kuwapa masharti magumu mtandao wa VEVO kwenye nchi ambazo haupatikani moja kwa moja kama Tanzania.

Unaweza ukasoma pia kujua tofauti ya Mtandao wa YouTube na VEVO  na jinsi wanavyofanya kazi kwa pamoja bonyeza link hii->Fahamu utofauti uliyopo kati ya VEVO na YouTube .

Ujio wa ‘Official Artist Channels’ utawanufaisha pia wasanii ambao kutokana na sababu za hapa na pale wamejikuta wamefungua akaunti mbili zote za YouTube kwani akaunti hizo zitaunganishwa kwa pamoja.

Kwanini nasema ni tishio kwa Wasanii wanaotumia mtandao wa VEVO?

YouTube wamesema video zote zilizopo kwenye akaunti ya VEVO zitakuwa kwenye channel moja ya ‘Official Artist Channels’ na hata subscribers watahamishwa na kuongezwa kwenye ukurasa mpya wa msanii.

Kiufupi ni kwamba hautaweza tena kusubscribe kwenye ukurasa wa msanii wa kawaida wa VEVO lakini video zake utaziona kama kawaida.

Je, itakuwa ndio mwisho wa Wasanii wanaotumia VEVO kwa nchi ambazo mtandao huo haupo bali unatumika kupitia YouTube kama Business Partner?

Jibu ni hapana kwani akaunti ya VEVO hutaiona moja kwa moja lakini msanii ataweza kuingiza kazi zake kama kawaida ila zitapatikana kwenye Channel hiyo ya ‘Official Artist Channels’ na hata ukisubscribe bado utakuwa umesubscribe channel ya YouTube ya Kawaida ingawaje video zote zilizopakuliwa na VEVO zitaonesha logo yao.

Tokeo la picha la VEVO

 

Zoezi hili ni kwa Wasanii wenye akaunti zaidi ya moja mfano Alikiba, Diamond Platnumz, Lady Gaga, Dj Khaled n.k . Na kwale ambao wana akaunti moja tu iwe ni ya VEVO au YouTube wataendelea kutumia kama kawaida.

YouTube wamesema mabadiliko hayo yataanza mwezi Februari mwaka huu na yamekuja baada ya kikao cha kupitia upya mikataba ya kibiashara na makampuni ya Sony Music Entertainment, Universal Music Group na Abu Dhabi Media kilichofanyika mwaka jana.

Lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuboresha mfumo wa udhibiti mapato ya Wanamuziki na Waandishi kwenye mtandao  (International Standard Name Identifier (ISNI) ) ambapo YouTube wamekuwa ndio mawakala rasmi wa kimataifa wa kusimamia zoezi hilo.

Tazama video ikielekeza mabadiliko hayo



 

Chanzo: bongo5.com