Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

You Tube waifungua Akaunti ya Trump

Trump Akaunti You Tube waifungua Akaunti ya Trump

Sat, 18 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtandao wa YouTube umeifungua akaunti ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump baada ya kuifungia kwa miaka miwili.

Hatua hiyo inalingana na ile iliyofanywa na Kampuni ya Meta inayomiliki Facebook na Instagram pamoja na mtandao wa Twitter unaomilikiwa na mfanyabiashara maarufu na tajiri namba moja duniani Elon Musk.

Rais Trump alifungiwa kuposti video kwenye mtandao wa YouTube mnamo Januari mwaka 2021 kwa kile walichokiita ni kuvunja sheria juu ya uchochezi wa vurugu.

Bado haijajulikana kama Trump ataendelea kuitumia akaunti hiyo kwani licha ya kufunguliwa kwa akaunti zake kadhaa za mitandao ya kijamii bado ameendelea kutozitumia.

Ijumaa iliyopita aliposti video fupi kwenye mtandao wa Facebook baada ya zaidi ya miaka miwili kupita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live