Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yote Maisha ya Madee na Stori ya kawli ya P-Funk na Kajala

Kajala P Funk(1) Yote Maisha ya Madee na Stori ya kawli ya P-Funk na Kajala

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Prodyuza mkongwe wa muziki P-Funk Majani na staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja wamewahi kuwa na uhusiano wa muda mrefu na kubahatika kupata mtoto wa kike, Paula.

Huyo alikuwa mtoto wa pili wa producer huyo wa Bongo Records na wa kwanza kwa Kajala.

Wimbo wa 'Yote Maisha' ni true story iliyomkuta P-Funk majani wakati akiwa na mahusiano na Kajala. P-Funk aliwasilisha hisia au maumivu aliyokuwa anayapitia wakati akiwa ana mahusiano na Kajala.

Na kipindi kumtumia rapa Madee kwa kuamini uwezo wa mshkaji huyo, kwa maana alikwisha kubali uwezo wa Madee kupitia kibao chake cha " Kazi Yake Mola".

Nanukuu kutoka kwa Madee;

“Mimi niliambiwa nifanye na Majani kwa hiyo hisia hizo unazoziskia ni hisia za P-Funk.”

“Haya Yote Maisha imetokea kipindi ambacho bado nipo na P Funk, halafu P Funk ana matatizo na mama mtoto wake Kajala. Kwa hiyo wakati mi naenda pale kurekodi cheza kidogo, kabla sijamalizana na ile nakutana na beat ya 'Yote Maisha' inaplay, halafu inaplay na chorus lakini hakuna verse.

Lakini the way ile beat inavyoplay majani anavyoiimba anaimba kwa feelings kinoma, nikamwambia bwana hii nyimbo mbona kali nigeie niimbe akasema hii na chana mwenyewe babu,” alisema Madee.

Madee aliendelea kusema baada ya mazungumzo P Funk alikubali kumpa beat na kwenda kuifanyia kazi, baada ya kukumbuka Madee mtindo alioutumia kwenye nyimbo zake.

“Sema wewe ulivyochana kwenye 'Kazi Yake Mola' kuna rhymes fulani naona unapita pita, unaongea kimajonzi hebu chukua hii beat kaandike. Kwa hiyo nikapewa ile beat, aliniambia kwamba hii nyimbo ina feeling zangu, nataka uandike kitu hiki na hiki, kwa hiyo idea iliyotoka mule ni idea ya P Funk,” alisema Madee akimuongelea P Funk Majani.

Lakini pia leo katika pitapita katika maktaba yangu nikakutana na kibao cha mwana Dada Madonna Msanii maarufu Dunia kinachoitwa 'Nothing really matters' kuna baadhi ya maishairi P Funk alitumia katika wimbo wa Madee 'Yote maisha'.

Wakati track ya yote maisha inaanza;

"Intro"

Utasikia maneno haya....

Now that I am grown Everything's changed I'll never be the same Because of you. Maneno haya pia yanapatikana katika wimbo wa Madonna " nothing really matters"

Swali: Je, nani alicopy idea ya mwezake, Madonna au Majani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live