Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yeyo Aipaisha Hip Hop Bongo Kimataifa

Dogo Hip Yeyo Aipaisha Hip Hop Bongo Kimataifa

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Hip Hop Mtanzania Yeyo 'The Miracle Kid' ametajwa mshindi wa mzunguko wa pili wa shindano maarufu 'Back The Mic' lililohusisha wasanii kutoka nchi kumi za Afrika.

Yeyo ameibuka na ushindi na kujizolea kitita cha Dola za Marekani 25,000 ambazo ni sawa na Tsh Milioni 58.

Mataifa mengine yaliyoingiza washiriki kwenye shindano hilo ni pamoja Nigeria, Rwanda, Kenya, Ethiopia, Afrika Kusini na Senegal. Huku Tanzania ikiwakilishwa na Yeyo Leon pamoja na Fresh like Uuhh.

Yeyo amebainisha wazi kuwa ushindi wake huo anauelekeza kwa mama yake mzazi marehemu Rosemarie Allan, aliyefariki mapema mwezi wa kwanza mwaka 2021 pamoja na dada yake aitwaye Debra ambaye aliyefariki karibu miaka mitano iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live