Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

'Yesu feki' azua gumzo mtaani

Yesu Feki.png 'Yesu feki' azua gumzo mtaani

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali ya kushangaza imejitokeza nchini Nigeria baada ya wakaazi Edo kumwona mtu waliyedai kuwa anafanana na 'Yesu. 'Yesu' yule wanaosema ni Yesu Kristo, Yesu wa Galilaya.

Video hiyo ya kuchekesha iliyoenea mtandaoni ikionyesha baadhi ya wakazi wa jiji la Benin, jimbo la Edo wakiremjelea mzungu huyo 'Yesu'.

Raia wa jimbo hilo walionekana kumjongelea,kumdhihaki na wengine wakicheka kutokana na kumfananisha na yule mcheza filamu za yesu.

Jamaa mmoja alisikika akimuita mzungu huyo kwamba; "Yesu wa Benin. Yesu kuja unisalimie."

Ila mzungu huyu kwa upole mwingi aliwafanyia ishara ya kufurahi kwa kutumia kidole gumba wakaazi huku akitabasabu licha ya kejeli hiyo.

Wanamitandao  hawakusazwa walipoiona video hiyo, kwani wengi walionekana kupungwa na klipu ile wakionesha kuhaha kutaka kukutanishwa na 'Yesu' yule.

"Yesu anakaa mtu wa kawaida. Nampenda," mmoja alisema.

"Mimi naamini Yesu alikufa na anaishi ndani yangu," mwingine alieleza imani yake.

"Yesu wangu sio mkonde kama huyu," mwingine alikejeli.

"Kama hujafurahia ungali humu nchini basi furaha haikuwa kusudio lako."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live