Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yemi Alade anusurika katika ajali ya gari Uhispania

Yemi Alade Anusurika Katika Ajali Ya Gari Uhispania Yemi Alade anusurika katika ajali ya gari Uhispania

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Mwimbaji na mtunzi maarufu wa nyimbo kutoka Nigeria Yemi Alade anasema amenusurika kwenye ajali ya gari alipokuwa nchini Uhispania.

Katika chapisho kwenye Instagram yake Jumanne,msanii huyo alifichua kuwa ajali hiyo ilitokea Alhamisi iliyopita akiwa safarini kati ya Barcelona na Benicassim.Hakuna vifo vilivyoripotiwa.

Alisema ajali hiyo "ilitokea ghafla" lakini alipata majeraha madogo,.

Alade, anayejulikana kwa muziki wake wa kusisimua, alisema licha ya ajali hiyo bado alitumbuiza jukwaani saa chache baadaye siku hiyo hiyo, kisha akapata "dharura ndogo ya matibabu" .

Alimshukuru Mungu kufuatia shida yake, akisema "Neema yake inatosha".

Chanzo: Bbc