Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yammi amtaka Nandy ageukie upande wake

Yammi Amtaka Nandy Ageukie Upande Wake Yammi amtaka Nandy ageukie upande wake

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Yammi ambaye anafanya kazi chini ya lebo ya ‘African Princess’, ameonesha kuchoka kusubiri kutoa kazi mpya na kuamua kumkumbusha boss wake ambaye ni Nandy ageukie upande wake.

Hayo yamekuja baada ya Nandy ‘kupost’ kwenye ukurasa wake wa Instagram, mafanikio ya ‘Dah remix’, aliyowashirikisha wasanii wa Hip-hop Joh Makini, Rosaree, GNako, Khaligraph, Moni na Stamina, huku akitaka kufanya remix na wasanii wa singeli.

Yammi aliijibu ‘posti’ hiyo kwa kuandika “kwa sasa inatosha sasa geukia upande wangu”.

Ikumbukwe kuwa Yammi mwezi uliopita alitoa wimbo uitwao ‘Love Crazy’ akiwa na wasanii Lexsil na ZiiBeats.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live