Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yaliyomtokea Dimpoz hata mimi yamenikuta- Ester

ESTER NA DIMPOZ Yaliyomtokea Dimpoz hata mimi yamenikuta- Ester

Sat, 17 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo anayefanya Bongo Movies, Ester Darwesh ametoa mtazamo wake kuhusu suala la Ommy Dimpoz kuwa asilaumiwe kwa sababu watu hawajui kilichopo moyoni mwake.

Ester ameyasema hayo Septemba 15, 2022 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV kuhusu masuala mbalimbali ambapo alipoulizwa kuhusu suala la Dimpoz kufunguka kuwa na matatizo na baba yake akasema watu wasimlaumu.

“Ommy anapaswa kutolaumiwa sababu yaliyomtokea hata mimi yalinitokea. Baba yangu alikuwa mwarabu lakini alinikataa tangu nikiwa mdogo.

“Mama yangu hakupandikiza chuki lakini mimi niliishuhudia mwenyewe chuki pale nilipoomba kuzungumza naye siku moja kupitia simu ya mama yangu, alimwambia hataki kabisa kuongea na mimi,” alisema Ester.

Jana Septemba 14, 2022 alipandisha kipande cha video kwenye ukurasa wake wa Instagram akielezea masikitiko yake kwa Clouds TV kumhoji baba yake mzazi ili kumfanya yeye aonekane hamjali mzazi wake wakati ukweli ni kwamba, baba yake hakumuonesha mapenzi tangu anazaliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live