Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Yafahamu maeneo matano hatari, yanayoogopesha zaidi Duniani

Maeneo Hatari 171.png Yafahamu maeneo matano hatari, yanayoogopesha zaidi Duniani

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dunia imesheheni maeneo mengi yenye kuvutia, mazuri, mahiri, ya kushangaza na hata mengine yenye muonekano wa kutisha, yanayoweza kukupa uoga au uhalisia wa maisha. Na kama unapenda kusafiri peke yako basi tambua kuwa yapo maeneo ambayo hutakiwi kujivinjari peke yako kwani yanaogofya.

Kisiwa cha Alcatraz, San Francisco San Francisco ni mji mahiri na mahali hapa ni maarufu kwa mambo kadhaa, kama vile, nyumba zake za rangi za ushindi, Daraja maarufu la Lango la Dhahabu na magari yanayovutwa na kebo, lakini je, unafahamu kuwa eneo hili ni la kuogofya? Wahalifu mashuhuri ambao waliwahi kuzuiliwa kwenye Kisiwa hiki cha Alcatraz wamekifanya kuwa maarufu.

Iwapo ungependa kutembelea hapa, unaweza kupanga ziara ya kuongozwa na mwenyeji ili kuyafahamu yote kuhusu maisha ya kuchukiza ya eneo hilo. Na zaidi ya hayo, safari za usiku ni hatari kwako kwani lolote linaweza kukutokea na hutakiwi kupuuza wala kwenda na mwenza wako wala usipaletee mzaha kwani eneo hili ni hatari kwa kuwa limejawa na matukio ya kuogofya ya kiuhalifu.

Kisiwa cha Poveglia, Venice, Italia Venice pia ipo kwenye orodha ya kuogofya, ni moja wapo ya maeneo mazuri ya kutembelea yanayopatikana Duniani. Lakini umewahi kusikia kuhusu Povelgia? hiki ni kisiwa kidogo kilichotelekezwa kilichopo kati ya mji wa Venice na Lido, ambacho kitakushangaza.

Kulingana na vyanzo mbalimbali vya Habari, eneo hili lililotelekezwa lilitumika kama kituo cha karantini ya tauni katika karne ya 20 na kisha katika miaka ya 1920 kama Hospitali ya magonjwa ya akili.

Ingawa kisiwa ni ngumu kupata mawasiliano, kuna kampuni kadhaa za watalii ambazo zitakupeleka huko na inadaiwa ukaaji wa muda mrefu wa magofu hayo umepelekea kuwa na matukio ya kuogofya yanayohusishwa na imani za giza na ni hatari kuyafikia bila kupata usaidizi wa wenyeji.

Kisiwa cha Dolls, Mexico Ingawa ni eneo maarufu na lenye mandhari mazuri, lakini mahali hapa panatisha na panaitwa Isla de las Munecas iliyo kusini mwa Jiji la Mexico, ikiwa na wanasesere wa kutisha wanaoning’inia kwenye miti na sauti za kuogofya.

Mamia ya maelfu ya watu wanaoishi karibu wanasimulia kuwa wanasesere hao wanawakilisha nafsi ya msichana ambaye inadaiwa alipatikana akiwa amefariki kwa kuzama maji kwenye kisiwa hiki miaka mingi iliyopita katika hali isiyojulikana.

Wanasema, wanasesere hao ukiwatazama au ukipita basi hugeuza vichwa vyao, kuchezesha mikono, na hata kuinua mboni za macho kisha kukutazama, swali ni kwamba kama hayo ni kweli je? wewe binafsi unaweza kuthubutu kwenda peke yako eneo hilo?

Kuldhara, Rajasthan Nadharia nyingi zenye utata zimeambatishwa mahali hapa nchini India, katika Kijiji hicho ambacho kimeachwa tangu miaka ya 1800, inaaminika kuwa kililaaniwa kutokana na tabia ya mtu mmoja aliyeanzisha chokochoko kwa raia.

Inadai kuwa, watu matajiri wa jamii ya Paliwal Brahmins waliwasili hapo na kuweka kambi ya kuishi katika eneo hilo ambapo baadaye ikatokea Waziri mmoja aliyeitwa Salim Singh aliwatishia kuwatoza Wanakijiji wazawa kodi kubwa mno la sivyo wamuache amuoe Binti mmoja mrembo wa Kijiji hicho.

Wenyeji walilaani kitendo hicho na walikesha usiku kucha wakimlinda msichana huyo dhidi ya Waziri huyo mwovu wakidai hakustahili kumuoa binti mdogo kiumri na badaye walifanikiwa kuhama naye na kukilaani Kijiji hicho.

Mpaka sasa hakuna mtu anayeweza kuishi kwa amani kutokana na mauzauza na hali mbaya ambayo bado ipo katika mji huo mdogo mpaka leo.

Kisiwa cha Wight, Uingereza Kinapatikana pwani ya kusini, eneo hili la kitalii linalovutia lina mandhari nzuri. Walakini, pia imejaa hadithi zisizo za kawaida na kila mwaka huuwa makumi ya maelfu ya “wawindaji vizuka” kutoka kote ulimwenguni ikidaiwa kafara za kibinadamu huhitajika na mizimu. Je, unaweza kuthubutu kwenda peke yako?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live