Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wolper awaonya wa watu wa mitandaoni

Wolper Pic Data Wolper awaonya wa watu wa mitandaoni

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Jaquiline Wolper, amesema amejipanga kushughulika na watu watakaomdhihaki mtoto wake mitandaoni bila kujali ukubwa wa mtu huyo.

Wolper ameyasema hayo leo Alhamisi Septemba 16, 2021 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni mara ya kwanza kuonyeshe sura ya mtoto wake huyo anayeitwa Pascal.

Wolper alijikuta akiyasema hayo baada ya kuulizwa namna gani amejipanga na mapokeo ya watu hususani wa mitandaoni ambao baadhi wamekuwa wakitoa lugha zisizo na staha pale wasanii wanapowaweka watoto wao mitandaoni.

Akijibu hilo, amesema amejipanga na wanasheria wake, endapo kuna mtu atajitokeza na kufanya hilo kwa mtoto wake watakutana kwenye vyombo vya sheria.

"Naomba niwaambie wanaopenda kuwazodoa watoto wa  watu mitandaoni, kwa mtoto wangu wasithubutu, nimejipanga vilivyo kukabiliana nao, kwa kufuata sheria kwa kuwa nikisema nijichukulie sheria mkononi nitajikuta namuacha mtoto wangu halafu mimi naishia ndani," amesema  Wolper.

Hata hivyo alitumia nafasi hiyo kuwashauri watu wenye tabia hizo kuacha mara moja na kueleza kama ni mwanamke au mwanaume ambaye naye ana  mtoto huyo atakuwa na laana yake na wale ambao hajajaliwa watoto awe baba  au mama siku wakipata watoto watajua uchungu wake.

Kutokana na hilo aliiomba jamii kuheshimu watoto wa wenzao bila kujali ni wa msanii au wa watu wa kawaida kwa kuwa nao wana haki zao kama binadamu wengine.

Akielezea sababu ya kumficha mtoto wake, amesema ilikuwa ni maamuzi jambo ambalo pia limemsaidia aonekane na wakati huohuo kuingiza pesa baada ya kupata ubalozi wa bidhaa za nguo za watoto.  

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz