Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wolper atoa darasa zito la maisha

Batch Wolper Wolper atoa darasa zito la maisha

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jacqueline Wolper; ni sataa wa Bongo Movies ambaye anasema kuwa, anajuta kwa kuwa alifanya kosa kujaza ndani kwake fenicha za zaidi ya shilingi milioni 50 wakati bado hajajenga nyumba yake.

Wolper anawataka Watanzania wanaoishi nyumba za kupanga kutumia fenicha za kawaida ili waweze kujenga nyumba zao haraka.

“Nakukumbusha tu kwamba usifanye makosa tuliyofanya sisi au niliyofanya mimi, unakuta mtu unakaa kwenye nyumba ya kupanga, lakini una fenicha za zaidi ya shilingi milioni 50 au milioni 60. “Mimi natoa mfano wangu mimi, kwa mfano nikiangalia kitanda, baa au kaunta ya kuwekea vinywaji, sijui sofa, nikijumlisha fenicha zote ni kama milioni 60 hivi au zaidi ya 50.

“Nakushauri, kama una pesa zako na unaishi kwenye nyumba ya kupanga, nunua fenicha za kawaida halafu hizo pesa nyingine jenga kwanza,” anasema Wolper au Mama P.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live