Muigizaji Jaqueline Wolper amefungukia madai ya kuchepuka na mpenzi wa Aunt Ezekiel, Kusah.
Wolper anasema alishtushwa na hizo habari lakini alijipa muda wa kutafakati kabla ya kuchukua uamuzi mbaya.
"Yule mdada ni mtu mzima (Maimartha) namheshimu nilishangaa sana anaibua madai kama hayo wakati anafahamu madhara yake, mimi nina wazazi wa pande zote mbili, nina watoto wawili hivyo sijui alifikiria nini kuzusha vile.
"Niliamua kukaa kimya maana unaweza kumpiga mtu akafa ukapelekwa jela na yeye akaenda kuzikwa. Nilikaa kimya lakini nikafatilia na kugundua alipewa nikamuuliza kwa nini hakutaka kuniuliza?," alihoji Wolper.