Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wolper: Siwezi kucheat

Batch Wolper Wolper

Sat, 9 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NYOTA wa Bongo Muvi Wolper amedai kuwa yeye hawezi kudanganya (kucheat) iwe katika mahusiano au katika mambo mengine ya msingi kama vile biashara au kazi.

Wolper anaelezea mikakati mbalimbali ya kazi zake za uigizaji amesema hawezi kufanya kazi za kuajiriwa zaidi ya moja kwani hawezi kujigawa ni vema afanye kazi yake binafsi na angalau moja ya kuajiriwa.

“Unajua kiukweli mimi siwezi kucheat kama ilivyo kwenye mahusiano, yaani siwezi kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja sawa napenda sana hela lakini siwezi kufanya huku na kule naweza kuwaharibia watu kazi zao.”

Sambamba na kuzungumzia mikakati yake lakini pia amesema mashabiki wa Bongo Muvi wategemee kazi nzuri na muda si mrefu yeye na waigizaji wenzake wataweka wazi kazi yao mpya kupitia mkutano na waandishi wa habari.

Wolper ameendelea kwa kusema kuwa kuna kazi inayotarajiwa kuwashirikisha wasanii mbalimbali maarufu wa uigizaji akiwemo Lulu, Kajala Masanja, Aunt Ezekiel, Dude na wengine wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live