Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wolper, Rich Mitindo kupata mtoto wa pili

Wolper Mimba Wolper, Rich Mitindo kupata mtoto wa pili

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Good news! Wapendanao Jacqueline Wolper na Rich Mitindo wanatarajia kupata mtoto mwingine baada ya mrembo huyo kuwa na mimba nyingine kubwa.

Hilo limethibitishwa na Rich Mitindo hii leo Agosti Mosi, 2022 baada ya kutupia picha inayomuonesha yeye akiwa na Wolper pamoja na mtoto wao wa kwanza.

Kwenye picha hiyo, tumbo la Wolper linaonekana live bila chenga kwamba tayari ni mjamzito. Kwenye picha hiyo, Mitindo amesindikiza na ujumbe uliosomeka hivi:

“Asante Mungu kwa hiii zawadi nyingine, Wakati tulipofikiri kwamba tumebarikiwa Mtoto wa Kwanza ajabu Mungu Kaonyesha Miujiza Yake nakutupa furaha nyingine nasubiri kwa hamu ujio wako, karibu sana mwanangu, Mama ako Anakupenda sana, Pia mim na Kaka ako maombi yetu yapo juu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live