Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wolper: Nimeitwa kulihubiri neno la Mungu

Wolper Mimba Wolper: Nimeitwa kulihubiri neno la Mungu

Sun, 11 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jaqueline Wolper Massawe au Mama P; ni staa mkubwa wa Bongo Movies ambaye ni miongoni mwa waigizaji wanaoshabikiwa mno kwenye tasnia ya filamu ya Tanzania kuanzia miaka ya 2000.

Safari hii Wolper anazungumziwa baada ya kudokeza kwamba amefikiria wakati anahisi kwamba upako wa Mungu umetua kichwani mwake na anahisi kama ameitwa kulihubiri neno la Mwenyezi Mungu.

Wolper anasema kwamba siku hizi kila baada ya kusikiliza nyimbo za Injili huingiwa na nguvu za ajabu zinazompa msukumo wa kutaka kumtumikia Mungu.

Wolper anaonekana kwenye video akifurahia wimbo ambao unachezwa kwenye mgahawa mmoja huku akijivinjari na kuimba sambamba na wimbo huo na kuifuatisha kwa maneno kwamba anahisi ni muda wa kumtumikia Mungu kwa nyimbo za Injili sasa.

“Kiukweli nafsi yangu inanituma kumtumikia Mungu wangu; yaani Nitoe ushuhuda na nimuimbie kwa sauti ya juu hadi wanyama wasikie; yaani nina hiyo roho na sijui imetoka wapi. Mungu tenda miujiza yako nikakutumikie wewe kuokoa vijana waliopotea,” anasema Wolper ambaye ni mama wa watoto wawili.

Wafuasi wake wengi walifurahia hatua hiyo na kumpongeza kwamba kama kweli roho wa Mungu amemtuma, basi asijaribu kukwepa kama Yona kwenye Biblia na ni sharti atii kile ambacho Mungu amemtuma kufanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live