Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizkid akunja bilioni 2 Tamasha la Rolling Loud

Wizkidshow News Wizkid

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa AfroPop kutoka pande za Nigeria Wizkid ametajwa kwenye orodha ya wasanii watatu vinara (headliners) ambao watatumbuiza kwenye tamasha la Rolling Loud ambalo litafanyika Septemba 9-11, mwaka huu mjini Toronto Canada.

Mbali na Wizkid kuna Future na Dave ambao ndio wanakamilisha idadi ya headliners watatu wa tamasha hilo lenye mamia ya wasanii wakali toka nchini Marekani ambao watapanda Jukwaani.

Kubwa hapa ni kiasi cha pesa ambacho Wizkid amelipwa kutumbuiza kama msanii kinara, kupitia insta story yake amesema amelipwa ($1 million) zaidi ya Shilingi Bilioni 2.3 za Kitanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live