Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Wivu kupita kiasi husababisha tatizo la afya ya akili kwa wanandoa

IMG 0452B (1) Wivu kupita kiasi husababisha tatizo la afya ya akili kwa wanandoa

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa vivu kupita kiasi kwa wanandoa na wapenzi huchangia watu kupata tatizo la afya ya akili na kusababisha kufanya matukio ya kikatili.

Hayo yalisemwa na mkurungenzi wa mahusiano Mayasa Kalinga kutoka Jukwaa la kupambana kuzuia tabia za watu kujinyonga Tanzania (TSPC).

Mayasa ambaye alitoa mada kwa washiriki wa semina za Jinsia na Maendeleo ( GDSS),mada iliyokuwa ikihusu,afya ya akili na wimbi la ukatili kwa wanandoa na wapenzi,alisema kuwa matukio ya kikatili yanaendelea kuwa wingi hapa nchini.

"Wivu kupita kiasi kwa wanandoa na wapenzi,husababisha watu kupata ugonjwa wa afya ya akili," alisema.

Aliongeza kuwa unyanyasaji ubaguzi na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wanawake,vimekuwa kichocheo katika kudorolesha afya ya akili kwa kwa wanawake.

Alisema takwimu za jeshi la polisi kuanzia Januari mwaka jana hadi mwezi Juni 2021 watu 15,131 walifanyiwa ukatili wa kijinsia .

"Kuhusu ripoti hiyo,ilionyesha ongezeko mauaji kwa wanawake walio katika ndoa," alisema.

Aliongeza kuwa matukio ya mauaji na ukatili wa kijinsia hasa kwa wanandoa yameendelea kuongezeka nchini Tanzania,hali iliyoibua sintofahamu kuhusu usalama wa hali ya Afya ya akili na usimamizi nchini Tanzania.

Aliongeza kuwa ripoti ya mwaka 2021ya mwezi Septemba iliyotolewa .na jarida la Afrika kuhusu hali ya ukatili wa kijinsia, Tanzania ni miongoni mwa wanandoa ambao ufanyiwa ukatili wa kijinsia.

"Asilimia 46 ya wanandoa hufanyiwa ukatili wa kijinsia, asilimia 36 walifanyiwa ukatili. wa kimwili,asilimia 32 walifanyiwa ukatili wa kisaikolojia na asilimia 13 walifanyiwa ukatili wa kingono," alisema.

Aliongeza kuwa kutokana na matukio ya kikatili kutokea kila mara,aliomba elimu ya Afya ya akili ianze kutolewa kuanzia shule za msingi hadi vyuoni.

Alisema Serikali iongeze bajeti kubwa katika afya ya akili kutokana na kutengwa kwa bajeti ndogo ya Afya ya akili.

"Kwa kuwa ugonjwa upo kwa jamii, Serikali inatakiwa iongeze bajeti hiyo,kiasi cha shilingi bilioni mbili kilichotengwa kwa ajili ya afya ya akili nikidogo kutokana na tatizo kuwa kubwa," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live