Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wimbo wa Harmonize "Sandakalawe" waondolewa YouTube

Kondepic Data Wimbo wa Harmonize "Sandakalawe" waondolewa YouTube

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Wimbo wa msanii wa Bongofleva kutoka Konde Music Worldwide, Harmonize uitwao Sandakalawe umeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na masuala ya hakimiliki.

Taarifa za mtandao huo zimeleeza kuwa kampuni ya usambazaji muziki 'Empire' imelalamika kuwa wimbo huo umechukua baadhi ya vionjo kutoka kwao.

Kutokana na hilo, wimbo huo umezuiwa hadi pale pande hizo mbili zitakapokaa na kukubalia. Hivyo kwa sasa mashabiki wa Harmonize nchini Tanzania hawataweza kuusikiliza wimbo huo kupitia YouTube. Si mara ya kwanza kwa Harmonize

Agosti mwaka jana Rosa Ree alimshtaki Harmonize kuchukua mdundo wa wimbo wake 'Kanyor Aleng' bila idhini yake na kuutumia katika wimbo wake uitwao Ameen jambo hilo likapelea wimbo huo kufutwa kwenye mtandao wa YouTube kwa kukiuka taratibu za hakimiliki.

Huo ulikuwa ni wimbo wa pili kwa Harmonize kuondolewa YouTube kutokana na mdundo wake kuonekana kunakiliwa kutoka kwenye wimbo fulani, wa kwanza ni Uno ambao Prodyuza wa Kenya, Magix Enga alipeleka malalamiko yake kwenye mtandao huo, kisha wakauondosha kwa muda. 

Pia albamu yake, Afro East iliwahi kufutwa kwenye mitandao mikubwa ya kuuza na kusikiliza muziki duniani kama Tidal, Amazon, Deezer, Yandex na YouTube Music kutokana na wimbo 'Your Body' ambao amemshirikisha Burna Boy kutokea Nigeria kuchukua vionjo kutoka kwenye wimbo wa Marehemu Papa Wemba uitwao Show me the Way, hiyo ni kutokana na kile inachodai hakuzingatia taratibu za hakimiliki.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz