Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Willy Paul awaonya warembo wanaomsumbua "Jovial ni mke wangu"

Willy Paul Jovial Willy Paul na Jovial

Thu, 29 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki maarufu nchini Kenya, Willy Paul amedai kuwa amezama katika mapenzi na mwanamuziki mwenzake Juliet Miriam Ayub maarufu kama Jovial.

Kupitia ujumbe aliyopisti katika akaunti yake ya Twitter, Willy Paul amesema kuwa yeye na Jovial sasa ni mume na mke licha ya wengi kuhoji kuwa ni kiki tu ya muda.

Willy amedai kuwa yeye na Jovial wanapendana kwa dhati kiasi cha kuwa familia na penzi lao haliwezi kusambaratishwa na yeyote.

"Hakuna kitu ambacho kitabadilika hata mkiongea, tushapendana na ni hivyo. Hii picha ya kifamilia iko aje?" Willy Paul alipakia ujumbe.

Willy Paul alionekana kukerwa na mashabiki wanaohoji uhusiano wao wa kimapenzi kuwa taifa la Kenya ni la ajabu sana.

Mwanamuziki huyo pia aliomba radhi kwa mabinti wote ambao walikuwa na matumani kuwa wangekuwa wachumba akisema kuwa hilo sasa limepitwa na wakati na haliwezekani tena.

“Kenya ndio mahali pekee ambapo ni jambo kubwa kuingia kwenye mapenzi!... Na kwa wale wasichana ambao labda tulikuwa na mazungumzo ambayo yalikuwa yanaendelea, poleni, nishapenda kwingine,” msanii huyo aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live