Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Willy Paul amsifia Rais Ruto kuwa mtumishi wa Mungu asiyedanganya

Willy Paul Amsifia Rais Ruto Kuwa Mtumishi Wa Mungu Asiyedanganya.png Willy Paul amsifia Rais Ruto kuwa mtumishi wa Mungu asiyedanganya

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mwanamuziki wa nyimbo za injili, Wilson Radido almaarufu Willy Paul amemsifia Rais Ruto akisema Rais hajai mdanganya mtu yeyote.

Willy Paul katika ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter, alimsifia Rais kwa kuwa mtu anayetimiza ahadi zake licha ya maoni ya mchekeshaji Eric Omondi kuwa hakuna ahadi ya serikali inayoongozwa na Ruto imetimizwa.

"Mpendwa Rais, najua wewe ni mwanaume anayetimiza ahadi yake. si hio peke yake, wewe ni mtu unayemwogopa Mungu sana. Watumishi wa Mungu hawadanganyi na sijawai kuona ukidanganya."

Mmiliki huyo wa lebo ya Saldido, aliyasema haya alipokuwa akimkumbusha Rais Ruto ahadi yake ya kufanya kazi naye kuimarisha sekta ya sanaa.

"Kumbuka ujumbe huu Rais. Tulielewana kushirikiana na ufanya tasnia ya burudani bora na kubwa. Sasa ni tayari kwa ofisi tuliyokuwa tumzunguzia."

Jumapili, Pozze amejivika jukumu la kuwa mshauri wa muziki na kuwashauri wanamuziki wa hapa nchini kuacha kufanya muziki kwa lugha ya kiswahili na kufanya muziki wao kwa kiswahili.

"Ushauri wangu kwa wanamuziki wa Kenya, tafadhali mzoee kuimba kwa kizungu."

Alisema wasanii kuimba kwa kiswahili kilikuwa kizuizi kikubwa kwa muziki wa Kenya kutofanya vyema nje ya mipaka ya Kenya. Aliongeza wasani hawa hawafahamu lugha ya kizungu lakini waweke jitihada.

"Hilo tu ndilo ambalo kinatuzuia kuvuka mipaka. Najua kuwa wasanii na kizungu ni maji na stima...hamjui lakini mjaribu tu na mkishindwa mtafute msaidizi wangu mpate msaada bila malipo."

Hivi majuzi Pozze alitangaza kuwa uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake wa zamani na aliyekuwa mwanamuziki wa lebo yake, Miss P. Willy Paul katika tangazo hilo aliwashauri wanawake kutuma maombi ya kutaka kuchumbiana naye.

"Ladies, Kwa vile mimi na Miss P Hatupo pamoja tena, nawahimiza sana mtume maombi yenu sasa. Orodha ni ndefu. Kumbuka, muda haumngojei Mwanamke yeyote."

Chanzo: Radio Jambo