Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Willow Smith: Sijapata mafanikio kupitia wazazi wangu

Willow Smith Willow Smith: Sijapata mafanikio kupitia wazazi wangu

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Willow Smith ambaye ni mtoto wa mwigizaji kutoka nchini Marekani, #WillSmith, ameweka wazi kuwa mafanikio aliyonayo hayatokani na wazazi wake bali ni juhudi zake mwenyewe.

Willow Smith wakati alipokuwa kwenye mahojiano na jarida la Allure, ameeleza kuwa watu wanafikiri sababu ya yeye kufanikiwa ni kutokana na wazazi wake jambo ambao siyo kweli kwani anaamini amepata mafanikio hayo kutokana na kupambania ndoto zake.

Aidha, aliongezea kwa kueleza kuwa hapo awali alitumia nguvu nyingi na bidii kujaribu kuwaonyesha wanaosema kuwa amepata mafanikio kupitia wazazi lakini sasa hatofanya hivyo tena ataacha kazi zake ziongee.

#WillowSmith ni mwigizaji pamoja na mwimbaji anatamba na ngoma zake kama ‘Wait a Minute’, ‘Whip My Hair’, ‘alone’ huku akionekana katika filamu kama ‘I Am Legend’, ‘A Man Named Scott’, na nyinginezo .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live