Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Will Smith amuomba radhi Chris Rock

Will Smith Chris Rock Slap Chris Rock

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji maarufu kutoka nchini Marekani Will Smith amemuomba msamaha mchekeshaji Chris Rock baada ya kumpiga kibao kwenye hafla ya tuzo za Oscar 2022, ambapo mara baada ya Smith kumpiga Chris Rock alisikika akisema ”usilitaje taje jina la mke wangu”

Will Smith ameomba msamaha huo kupitia mtandao wa Instagram ambapo Smith ameposti video fupi huku akisema "nimekuwa nikifikiria sana tangu siku ile"

"Chris, ninaomba radhi. Tabia yangu ilikuwa haikubaliki. Niko hapa wakati wowote utakapokuwa tayari kuongea."

Smith amekiri kumtafuta Rock lakini ujumbe aliojibiwa ni kuwa "siko tayari kuongea".

Smith ameiomba radhi pia familia ya Rock kipekee kabisa mama yake mzazi, kutokana na tukio hilo lililojitokeza baina ya wawili hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live