Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wiki 2 tu Gigy huru

Gigy Pic Data Wiki 2 tu Gigy huru

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

HATIMAYE miezi sita inaenda kukatika tangu msanii Gift Stanford ‘Gigy Money’ kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kujihusisha na sanaa ndani na nje ya nchi.

Gigy alifungiwa Januari 5 mwaka huu na baraza hilo ambalo lilieleza kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya Gigy kutumbuiza akiwa hajajisitiri katika tamasha la ‘Tumewasha Tour’ jijini Dodoma.

Ilibainisha kuwa kitendo hicho kilidhalilisha utu wa msanii huyo na kubughudhi hadhira ya wapenda sanaa ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo, tayari miezi hiyo imekatika na sasa zimebaki wiki mbili kwa msanii huyo kuwa huru.

Kipindi chote hicho Gigy amekuwa akipambana ili kufunguliwa ikiwemo kwenda kwenye taasisi yao ya Chama cha Wasanii wa Kizazi Kipya (TUMA), kuomba wamsaidie.

Pia alikuwa akitumia mitandao ya kijamii kuomba huruma hiyo lakini bado haikufua dafu, kwani Basata ilisimamia msimamo wake kuwa alipaswa kufuata taratibu ya kuandika barua kwa Waziri mwenye dhamana na sanaa aidha kuomba kupunguziwa adhabu au kukata rufaa ya kutoridhika na adhabau hiyo, jambo ambalo Gigy hakufanya.

Akilizungumzia hilo, Katibu wa Tuma, Samuel Andrew ’Braton’, alikiri Gigy kuomba msaada kwao, na kueleza kuwa kwa muda uliobaki bado wanajifikiria aidha waache tu amalizie adhabu kwa kuwa zimebaki siku chache au wamuone Waziri kujadili hilo.

Gigy amejiunga na TUMA hata hivyo mpaka sasa bado kuna baadhi ya taratibu hajazikamilisha.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz