Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Whozu ampigia simu Wema live kumuuliza kama amemtema

Wema Whozuu Ms(1) Whozu ampigia simu Wema live kumuuliza kama amemtema

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya uvumi kuenezwa mitandaoni kuhusu msanii Whozu kupigwa buti na mpenzi wake muigizaji Wema Sepetu, msanii huyo ameamua kuthibitisha hili kwa mashabiki wake moja kwa moja kwenye kamera.

Whozu alirekodi video akiwa kwenye gari akimpiga Wema Sepetu kumuuliza kuhusu uvumi huo ambao hata yeye alidai aliuona mitandaoni bila.

Dhumni la kumpigia Wema simu lilikuwa ni kuhakiki kama ni kweli Wema amemuacha kama inavyosadikika mitandaoni au ni choyo ya watu tu wasiopenda kuwaona pamoja. Whozu alisema kwamba katika siku za hivi karibuni, Wema amekuwa akiandika kauli za kumchamba mtu ambazo zilitafsiriwa kwamba zinamlenga yeye.

“Nashangaa watu wanasema umeachana na mimi, umeandika vichambo vile vimenilenga mimi, wewe kumbe umeniacha halafu husemi. Mambo umeandika huku watu wanasema moja kwa moja umeachana na mimi sasa mbona usifafanue mimi mambo ya kiki siyawezi jamani,” Whozu alimlalamikia.

Wema alikanusha kuachana na yeye akisema kwamba wambea siku zote hawakosi la kuamba, akisema kwamab aliyoyaandika mitandaoni ni maudhui baada ya kuwahoji watu kuhusu kipindi chake katika kituo kimoja cha redio anachokiongoza yeye.

“Akha, sasa wewe nimeachana na wewe lini, kwani mimi nimekuambia nimeachana na wewe? Si tunaongea na wewe saa zote. Mimi sina wanaume wengine, hayo maneno ni ya Zanzibar huku tumeenda tumekaa tumehoji watu wanaongea maneno yao,” Wema alisema.

Wawili hao wamekuwa wakichumbiana tangu mapema mwaka jana licha ya kuwepo kwa pingamizi kali kutoka kwa mashabiki haswa kuhusu kigezo cha umri wao, Wema akiwa anamzidi Whozu kiumri mara dufu.

Hata hivyo, wema kwa wakati mmoja alipakia klipu kwenye Wema App akikiri kwamba penzi lake na Whozu halitoenda mpaka kufikia hatua ya kupata watoto au kufunga harusi, akiashiria kwamba Whozu ni wa kumpa faraja tu wakati ambapo dunia nzima inamsimanga kwa juhudi zake za kujaribu kupata mtoto kufeli baada ya majaribio ya muda mrefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live