Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Whozu, Tunda, Wema hali ya hewa imechafuka

Wema Na Whozu Whozu, Tunda, Wema hali ya hewa imechafuka

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Whozu amefunguka kwa mara ya kwanza kinachoendelea kati yake na Wema Sepetu ambaye ni mpenzi wake baada ya kudaiwa kumpiga, jambo lililosababisha ugomvi baina yao na kuzua mijadala katika mitandao.

Whozu amekiri kuwa hawako sawa na Wema na ni kitu cha kawaida na kusema hapendezwi na maneno aliyoyasema Mzazi mwenzake Tunda kuwa bado anampenda na kuna Watu Whozu anawatuma kwa Tunda kitu ambacho kinaharibu mahusiano yake.

Whuzo pia ameongezea kwa kusema; "Mimi na Wema ni ishu za mapenzi yakizidi kuna kufuatiliana, kupigana, sababu ya kupenda, sitopenda kuongelea sana, sijafuta picha za Chimama ina maana kuna amani, Watu wajue nampenda sana Wema," amesema Whuzo.

Aidha, msanii huyo amemtolea uvivu mzazi mwenzake Tunda akidai kuwa; "Sijawahi kumtafuta Tunda kimapenzi zaidi ya masuala ya mtoto, Tunda amedanganya na isitoshe simpendi," amesema Whozu na kumaliza kuwa anafakiria kuacha kuwasiliana na Tunda hata kwa masuala ya mtoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live