Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Whozu: Nimejifunza kitu

Whozuuu Whozu: Nimejifunza kitu

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Staa Oscar John Lelo maarufu Whozu amesema kupitia msamaha aliopewa wa kuruhusiwa kuendelea kufanya kazi zake za sanaa baada ya awali kufungiwa kwa miezi sita, amejifunza na ameshukuru Serikali kwa msamaha huo.

Whozu amesema hayo leo baada ya kumalizika kwa kikao cha kusikiliza rufaa yake na wenzake, Billnass na Mbosso ambacho kimefikia maamuzi ya kuwataka Wasanii hao kulipa faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi za sanaa nchini kwa kufuata maadili ya Kitanzania.

Whozu anatakiwa kulipa faini ya Tsh milioni 5, Billnass Tsh milioni moja huku Mboso akitakiwa kulipa milioni tatu na wote kwa pamoja wameondolewa adhabu za kufungiwa.

Itakumbukwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lilimtaka Msanii Whozu kushusha mara moja video ya wimbo wake wa ‘Ameyatimba’ kwenye digital platform zote, pia likamtoza faini ya Tsh milioni 3 na kumfungia kujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi 6 kuanzia November 04, 2023 kutokana na wimbo huo kuwa na maudhui yanayokiuka kanuni za maadili.

BASATA ilisema Whozu alichapisha video ya wimbo huo Nov 02, 2023 akiwashirikisha wasanii wenzake Mbosso na Bill Nass, na kwamba wimbo huo una maudhui yanayokiuka kanuni za maadili kutokana na kuwepo ishara ya vitendo vinavyoashiria matusi kinyume na Kanuni ya 25(6) (j) pamoja na vitendo ya unyanyasaji, ukatili na udhalilisha wa utu wa Mwanamke kinyume na Kanuni ya 25(6)-(f).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live