Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Whozu Aanika Sababu za Kumficha Mwanaye

Whozu Mtoto Whozu Aanika Sababu za Kumficha Mwanaye

Thu, 6 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara ya kwanza msanii Whozu 'Don Dingoo' amenyoosha maelezo ya chanzo cha kumficha mtoto wake Lola aliyempata na mrembo Cappuccino Tunda.

Whozu ameshea video clip ya mtoto wake kwenye ukurasa wake wa Instagram kisha kuandika ujumbe ufuatao.

"Lola mrembo wangu baba yako nilikuficha sana nilitaka ukue vizuri ila walimwengu bahati mbaya wamenizidi nguvu, sisi tumeshaamua kumtegemea Mwenyezi Mungu tu".

"Nikwambie tu mwanangu Instagram ni maisha ya teknolojia utasifiwa, utatukanwa, utaambiwa kila kitu, hilo wala lisikuumize kichwa kwanza sio shida zako mwanangu. Mimi baba yako nipo nyuma yako kwa lolote lile".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live