Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema hana gari, Uwoya kalipataje?

Wema Sepetu Wema hana gari, Uwoya kalipataje?

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NI ajabu kuona nchi inafanya ishu ya mtu kutokuwa na gari kuwa mjadala hata wakubwa wanaingilia kati kuujadili.

Mtu anayejiita sijui Aristote amemwambia msanii Wema Sepetu kuwa hana gari na kwamba anatembelea ya kukodisha.

Akatia chumvi taarifa yake kwa kusema, Wema hana fedha kama alizonazo msanii mwenzake, Irene Uwoya ambaye anatembelea Range Rover; hilo tayari likawa kosa.

Muda mfupi baada ya taarifa hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikageuka kuwa mjadala wa kitaifa.

Shinikizo likawa Aristote akamatwe kwa udhalilishaji. Hivi, mtu akikuambia “huna gari” na kweli ukawa huna gari anakuwa kakudhalilisha katika mazingira gani? Wanasheria mnaweza kutusaidia tusioelewa mambo.

Kwa mtu mwelewa hawezi kulizwa na kauli ya mtu anayemwambia kuwa hana fedha na kweli akawa hana, zaidi sana kauli hiyo ataigeuza kuwa chachu ya kutafuta fedha ili amzibe mdomo aliyekuwa anamuona fukara.

Lakini cha kushangaza katika mjadala huu, kati ya Wema na Aristote ilionekana kuwa Wema kadhalilishwa na mwenyewe alisema ameumia na amelia sana kwa kuandamwa.

Watetezi wake wakiwemo baadhi ya viongozi wa serikali waliibuka mitandaoni na kumpa pole huku wakitaka Aristote akamatwe na polisi na kufunguliwa mashitaka.

Ndugu yangu; katika nchi hii ni wangapi hawana magari na wameambiwa hawana lakini hawakupata watetezi wa haki za binadamu ikiwa kweli kukosa gari ni udhalili?

Tanzania kuna maskini wangapi na kila siku wanaambiwa hivyo lakini hatuoni watu maarufu wakijitokeza na kuwapigania kwa kutoa povu la maana kwenye mitandao ya kijamii?

Yaliyo nyuma ya sakata la Wema mengi yamefichwa, pengine wengine hatuyafahamu ndiyo maana tunaona nyotanyota tu katika hili linaloendelea mitandaoni.

Wakati nahitimisha hoja ya kwanza niwaulize ambao walikuwa wanataka kumtetea Wema kama “mwanamke ambaye hana gari” walitaka kumuambia nini?

Maana nina hakika kuwa Wema anamfahamu vilivyo Irene Uwoya na maisha yake; anaposikia mwenzake anasifiwa anaishia kuachama mdomo na kujiuliza “nimekosea wapi?” Niwatake kwa lugha ya upole wale wanaomsifia Irene Uwoya kuwa anatembelea gari la kisasa wamuulize basi “amelipataje?”

Kufanya hivyo kunaweza kuwa msaada siyo kwa Wema pekee lakini kwa wanawake wengine wasiokuwa na magari na kwamba wanaishi kwa kutumia usafiri wa umma.

Wakifahamu huyu Irene ambaye hana kazi maalumu hapa mjini lakini anaishi maisha ya kifahari na kumwagamwaga fedha anatumia ufundi gani kuzichanga noti, wanaweza nao wakatumia akili hiyo kujikomboa na kile kinachoitwa ‘aibu ya kukosa gari’.

Lakini ikiwa Irene anacheza na dunia na kumpenda shetani na mambo yake, hivyo kumfanya apate fedha kwa mlango wa kushoto basi ni heri mara mia kuishi maisha ya kimaskini lakini yenye kuuheshimu utu pamoja na Mungu wako kuliko hayo ninayowaza kuhusu Irene Uwoya.

Kwa leo sina la kusema kwa vile nilishapoteza ukaribu na Irene Uwoya miaka mingi iliyopita hivyo sijui kwa sasa anaishije mjini na hili gari kalipataje.

Ninachojua ni kwamba hana kazi maalum hapa mjini hata yenye ofisi ya makuti. Watu wake wa karibu wanisaidie kumuuliza fedha anapata kupitia michongo gani?

Kama ni njia halali anastahili kusifiwa na kupongezwa lakini kama ni njia za dhambi, Irene anastahili kudharauliwa pamoja na gari lake na heshima iwe juu ya Wema mpanda ‘matatu’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live