Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema azidi kuteswa na kauli ya mama'ke, afunguka tena

Wema Azidi Kuteswa Na Kauli Ya Mama'ke, Afunguka Tena Wema azidi kuteswa na kauli ya mama'ke, afunguka tena

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji maarufu wa Tanzania Wema Sepetu ameweka posti ya kihisia siku chache baada ya mama yake Mariam Sepetu kumzomea hadharani wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika wiki iliyopita.

Siku ya Alhamisi, wiki jana, Bi Mariam alipokuwa akitoa hotuba yake wakati wa karamu ya bintiye alimkosoa kuhusu uhusiano wake na mwimbaji Whozu akitaja kuwa haukubarikiwa.

Chapisho la Wema Sepetu la Alhamisi jioni linadokeza kuwa tukio la wiki iliyopita lilimuumiza sana muigizaji huyo na kumuacha na majeraha moyoni.

"Sidhani mchakato wa uponyaji utaisha. Nadhani inakuja wakati ambapo utaamua kuwa majeraha yako hayatakuzuia kuwa mtu unayetaka kuwa. Upendo wa kibinafsi ni safari ya maisha yote na wakati mwingine ni mbaya zaidi kuliko wengine. Lazima tu ujitolee,” ulisema ujumbe ambao ulichapishwa na Wema Sepetu kwenye akaunti yake ya Instagram.

Miss Tanzania huyo wa zamani aliendelea kutangaza kuwa atazungumza zaidi Jumapili, tarehe 8, Oktoba.

Kumekuwa na tetesi kuwa Wema na Whozu hawajakuwa na uhusiano mzuri tangu mama wa muigizaji huyo kumuaibisha hadharani kuhusu uhusiano wao. Wawili hao hata hivyo bado hawajathibitisha hali ya uhusiano wao na huenda Wema atazungumzia hilo Jumapili.

Alhamisi wiki jana, Wema alibaki ameduwaa baada ya mamake kumkemea kwa kujivunia mahusiano na mwanaume ambaye hajatambulishwa rasmi kwenye familia..

Bi Mariam Sepetu alifichua kuwa alihisi kutoheshimiwa na bintiye na mpenzi wake kwani walikuwa wameweka uhusiano wao hadharani bila hata kutafuta baraka zake.

Aliendelea kuongeza kuwa ukiwa mtoto ni jambo la msingi kuwajulisha wazazi wako una uhusiano na nani na kumfahamu mtu ambaye una uhusiano naye.

"Nataka heshima itawale. Nataka wazazi waheshimiwe kama mtoto, lazima umsikilize mzazi wako. Kwa mpenzi ni lazima uje kujitambulisha," alisema Mariam kwa hasira.

Bi Mariam alifafanua kuwa hakuwa akijaribu kuelekeza maisha ya bintiye au kumzuia kupata mapenzi ila alichokuwa akiomba ni heshima tu, bila kulazimika kujua undani wa maisha ya bintiye mtandaoni.

Aidha, alishikilia kuwa alikuwa akifanya haya yote kwa sababu ya upendo mkubwa alionao kwa binti yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live