Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema awaomba radhi mashabiki wake

Ae144967ba78a790c4bf12f3db8fddfd Wema awaomba radhi mashabiki wake

Sat, 19 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi mashabiki zake baada ya kuahidi kurudi kwa msimu wa pili wa kipindi chake cha Cook with Wema, ambacho alihidi kuwa na mabadiliko makubwa .

Wema alisema kipindi hicho kilichoanza kuruka wiki hii kwa msimu wa pili, alitegemea angeweza kukifanyia mabadiliko lakini imeshindikana, hata hivyo anatarajia vipindi hivi vitaenda kwa wiki mbili kabla ya kuja kwa hayo mabadiliko.

Alisema tayari ameshafanya vipindi vingi, ambapo anaamini vipo kwenye mikakati ya mwisho kabla kuingia sokoni, kupitia mtandao wake wa kijamii, ambao umekuwa ukipatikana kupitia simu za mkononi.

“Kwanza kabisa nitoe shukran zangu za dhati kwa kuendelea kuniunga mkono na kuendelea kuwa shabiki zangu wazuri.

Niliwaahidi kuwa tunarudi kivingine kabisa na msimu wa pili, lakini naomba tu mniwie radhi kuwa sio kipindi hiki,” alisema

Chanzo: habarileo.co.tz