Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema avunja ukimya penzi la Whozu "Umenipa amani ya moyo, nakuita My Baby"

Wema Whozzu Bn Wema aanika penzi la Whozu

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni saa chache baada ya kuvujisha video yao ya mahaba tena mazito, Malkia wa Bongo Movies, Wema Sepetu amewatolea povu watu wanaoponda penzi lake na msanii wa Bongo Fleva, Whozu.

Video inayotrend mjini kwa sasa, inamuonesha Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 akibusiana mdomo kwa mdomo na Whozu huku wakiwa kwenye hafla fupi ya Birthday ya Wema.

Kupitia ukurasa wake, msanii Whozu ameposti video hiyo na kuandika maneno haya; “�???????? Am so happy when Chi Mama akiwa na furaha. Kwa sababu muda wake mwingi anatumia kufurahi.

“Hapendi kukosa raha, hapendi kukosa amani. ???? Thank God hata kwa hili nimeiongeza furaha yake siku yake ya yakuzaliwa. See how she’s happy… ???? HAPPY BIRTHDAY CHI MAMA❤️ You Know How much I love You Right.!! Enjoy your Day. @wemasepetu #ChiMama,” amesema Whozu.

Baada ya kauli hiyop ya Whozu, mashabiki walianza kuuponda uhusiano huo jambo ambalo limemuibua Wema na kujibu kwa ku-comment kupitia posti hiyo akisema kuwa;

“Umekuwa faraja yangu kubwa sana Chibaba wangu. Umenipa amani ya moyo sijapata kwa muda mrefu mnooo. Wewe ndo furaha yangu kwa sasa. Umegusa maisha yangu kwa namna ambayo sijawahi hata kudhani.

“Tokea nakujua kama rafiki mpaka dakika hii nakuita "My Baby". Hata sijui tumefikaje fikaje hapa tulipo ila nachoweza sema ni kwamba najiona ni Miongoni mwa wanawake Happy sana Duniani. Alhamdulillah for you.

"And thank you for loving me & always being there for me. Umenipa Glow ya hatari. Mungu aendelee kukuweka sana kwa ajili yangu❤️,” ameandika Wema.

Endapo itakuwa tukio hili sio kiki, Wema atakuwa amemnasa Whozu baada ya kuachana na Tunda. Tunda kwa sasa yupo kwenye mahaba mazito Meja Kunta.



View this post on Instagram

A post shared by Tanzania Web (@tanzaniaweb)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live