Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema aupiga mwingi kimyakimya

Wemaaa Wema aupiga mwingi kimyakimya

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wema Isaac Sepetu au Last Born wa Taifa; ni supastaa wa filamu nchini Tanzania ambaye anaupiga mwingi kwa kuungana na Serikali na kushiriki kuhamasisha watu na kuwapa chanjo ya UVIKO-19.

Kwa mujibu wa Wema, kwa wiki kadhaa, Wema na timu yake wamekuwa mikoa ya Kusini mwa Tanzania ya Lindi na Mtwara wakihamasisha na kuchanja watu ambapo muitikio umekuwa ni mkubwa hasa kwa vijana ambao wengi ni mashabiki wake na wanampenda hivyo wanamsikiliza anachowaambia.

Kila anakopita kauli yake ni hii; “Ujanja ni kuchanja na hii ni bega kwa bega, safari hii hatuachi mtu kila kata na wilaya ambayo muziki mnene utapita ni lazima na mimi nipite kutoa elimu ya afya pamoja na chanjo ya UVIKO-19…”

Baadhi ya wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii wanasema Wema na timu yake wamefanikiwa na hasa vijana mtaani wamevutiwa sana kumuona Wema ambaye wanamuona ni kivutio.

Wengi wa wafuasi hao wanamuomba Wema awatembelee na kuwachanja kwani hawawezi kugoma kuchanja kabisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live