Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema atambulishwa kwa wazazi wa Whozu

Whozu X Wema Sepenga Wema Sepetu

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa filamu Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amesema kuwa tayari mpenzi wake, Whozu amemtambulisha ukweni!.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Wema Sepetu aliulizwa ni lini atatambulishwa ndipo akajibu tayari.

“Kwani unadhani kwao hawanijui?” alisema Wema Sepetu ambaye hivi karibuni alikaririwa akisema anapenda kupata mtoto wa kiume.

Hata hivyo, Wema alisema kwa sasa yuko katika hali bora zaidi kwani kwa muda mrefu amekuwa pweke, jambo ambalo limemnyima furaha.

“Napenda sana kuonyesha hisia zangu, nikipenda napenda, nikichukia nachukia. Siwezi kujifanya, nadhani kwa muda mrefu nimekuwa sijapenda na sijakuwa na furaha,” alisema Wema.

Utakumbuka Wema Sepetu amewahi kuwa na mahusiano na Mastaa Bongo kama Diamond Platnumz, Mr. Blue, TID, Idris Sultan n.k.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live