Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema atamba kuwafunika wanawake wote Bongo

Wema Wanawake Wema Sepetu

Fri, 23 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa Wema Sepetu ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006 ni habari nyingine, nyota huyo ambaye ana miaka zaidi 16 kwenye gemu ni miongoni mwa mastaa wa kike nchini waliyodumu kwenye kiwanda cha burudani kwa muda mrefu akiwa bado anaendelea kusumbua.

Good news kwa mashabiki wa Wema ni kwamba amefanikiwa kufikisha followers Milioni 10 kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram na kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kufanya hivyo.

Aidha, Wema amebainisha kwamba hataki kushindanishwa na yeyote yule kwani naye hajawahi kushindana na mtu. Ameeleza kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuongoza kuwa na followers wengi kwa wanawake nchini.

"Thank You For 10M Followers By The way vipenzi vyangu... Nabaki kuwa wa kike wa kwanza Tanzania kufikisha 10M, basi naombeni kuanzia sasa, msinishindanishe na mtu jamani. Atakaefuata na kunizidi isiwe battle basi wapenzi wangu. Tumefikisha 10M bila nguvu yoyote, nitumie tu nafasi hii kusema ASANTENI na NAWAPENDA. ❤️????❤️" amesema Wema.

Fahamu, anayemfuata Wema ama kumkaribia ni mwanamitindo Hamisa Mobetto ambaye ana followers Milioni 9.9, kisha Shilole mwenye followers Milioni 9.4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live