Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema amkumbuka baba yake: Mpenzi wangu wa kweli, nakumiss sana!

WEMA SEPETU NA MZEE SEPETU Wema: Mpenzi wangu wa kweli wa kwanza, nakumiss baba

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku kama ya jana, baba ya muigizaji wa Bongo Wema Sepetu, marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu angekuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Bw Sepetu ambaye aliaga dunia takriban miaka tisa iliyopita alizaliwa Oktoba 16, miongo mingi iliyopita. Alifariki mnamo tarehe 27 Oktoba mwaka wa 2013 baada ya kupambana na ugonjwa wa kisukari na kiharusi kwa kipindi kirefu.

Muigizaji Wema Sepetu ametumia siku ya leo kumkumbuka marehemu baba yake na kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

"Kheri ya siku ya kuzaliwa kwa mwenzangu wa Libra, baba yangu Sepetu.. Mpenzi wangu halisi wa kwanza," aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mpenzi huyo wa mwimbaji Whozu alimtakia marehemu babake mapumziko ya amani na kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Endelea kupumzika baba angu mimi.. Nakupenda kila siku .. Nakumiss kila siku.. Nakumiss kila wakati.. Naendelea kukuombea sana," alisema.

Aliongeza "Allah akupunguzie adhabu za kaburi.. Amen????????????❤❤❤,"

Muigizaji huyo aliambatanisha ujumbe wake na picha kadhaa za kumbukumbu za mzazi huyo wake ambaye aliaga.

Bw Sepetu alifariki katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, Tanzania ambako alikuwa akipokea matibabu. Baada ya kuaga, marehemu alizikwa nyumbani kwake katika maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar es Salam.

Bw Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje katika miaka ya 1970 wakati wa utawala wa muhula wa kwanza wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.

Kufikia kufariki kwake, Bw Sepetu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live