Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema amcharukia shabiki aliyemuita 'Chawote'

Wemaaa Wema amcharukia shabiki aliyemuita 'Chawote'

Thu, 13 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Movies, Wema Sepetu alianika picha inayoonyesha akifurahia maisha na mpenzi wake mpya kwenye mitandao ya kijamii.

Shabiki mmoja aliingia kwenye sehemu ya maoni na kumtaja kama 'chawote', kumaanisha ni kiruka njia.

Hata hivyo, Wema alimtaka shabiki huyo amtaje mpenzi wake wa awali na kulalamika kuwa watu wamezoea kumuingilia.

Mwigizaji wa Tanzania Wema Sepetu ameingia kwenye penzi tena na haoni haya kuyaonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

Kisura huyo ambaye alikuwa mpenzi wa Diamond Platnumz, alianika picha yake akijivinjari na mahabubu wake mpya kwenye Instagram.

Kama ilivyotarajiwa, picha ilizua mjadala kubwa; zote chanya na hasi. Lakini mojawapo ya maoni ambayo yalimvutia Wema ni ya shabiki mmoja aliyemtaja kwa jina la “chawote” (neno la Kiswahili lenye maana ya wote).

Shabiki huyo alisema; "Huyo ndo @wemasepetu Chawote."

Wema hakuchuchelewa kwani alimtaka shabiki huyo kumuanika pia mpenzi wake waliyetengana. Alimuuliza shabiki huyo iwapo hakutaka apende mtu mwingine au apendwe.

"Hapo kati nilikuwa Cha nani? Kunionea tu muda wote... Mlikuwa mnataka nisipende tena au nisipende... Gimme a Break plz," alijibu.

Mnamo Februari 2022, Wema Sepetu alijibu madai kuwa amekuwa akitumia teksi kwa miaka mingi kwani hana uwezo wa kumudu gari.

Wema alisema ana haki ya kuishi anavyotaka. Nyota huyo wa Bongohood pia alibainisha kuwa hajali watu wengine wanafikiri na kusema nini juu yake.

Hivi ndivyo alivyojibu madai hayo: "Hivi nikitumia teksi, ni maisha yangu mwenyewe na maadamu niko sawa nayo, sijali sana. Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake. Watu wanaweza kuzungumza wanavyotaka kwa sababu ni kawaida kuzungumza juu ya wengine.

"Pia nawaongelea watu wengine lakini sio lazima umjulishe mtu unachomsengenya.Kama ndicho kinachomfurahisha mwache aendelee lakini sijali ilimradi hainigharimu chochote."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live